Huu ndo waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Dr. Kitila marakani- CHADEMA by @UC Browser http://mzalendoforum.com/showthread.php?tid=80
Jumamosi, 23 Novemba 2013
Ijumaa, 22 Novemba 2013
Yametimiaa
Baada ya CHADEMA kumvua uongozi Zitto Kabwe, Makamu mwenyekiti wa CHADEMA bara naye aamua kujiuzulu
Habari zilizotufikia muda mfupi ulipita zinaarifu kwa Said Arfi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA amejiuzulu rasmi nafasi yake jioni hii.
Arfi ambaye pia ni mbunge wa Mpanda mjini (CHADEMA) amefikia uamuzi huo leo baada ya Kamati Kuu ya CHADEMA kuwavua uongozi Zitto Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo. Nafasi ya Zitto amepewa mchungaji Peter Msigwa.
Ifuatayo ni kauli ya mwenyekiti huyo:
-------------------------------------------------------
KUJIUZULU MAKAMU MWENYEKITI (BARA)
Salaam,
Napenda kuwasilisha kwako taarifa ya kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa kuchoshwa na Unafiki unaoendelea ndani ya Chama. Napenda ifahamike pia kwangu maslahi ya Wapiga kura, Wakaazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa marafiki.
Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka mahusiano yangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu pamoja na kulijadili katika vikao kadha Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa. Hayo yalikua maamuzi ya Wanampanda kwenu imekua ni tatizo lakin hamsemi kwa nini Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa .Mlikua wapi na nani alaaumiwe huu ni Unafiki wa kupindukia.
Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe Mtei kutuchagulia viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa Mali binafsi
Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu
Said A Arfi (mb)
Nakala Vyombo vya Habari
Ijumaa, 8 Novemba 2013
KWA MARA YA. PILI NDA NI YA MWAKA MMOJA RAIS ANAHUTUPIA BUNGE. LA TANZANIA
Ijumaa, 1 Novemba 2013
WIZARA YA ELIMU TENA
Jumatano, 30 Oktoba 2013
UKISIKILIZA KILA MTETEZI UTADUWAA
Yametimia YANI HAONI KUNDULE
MPEKUZI: Uozo wa CHADEMA wajulikana...Hapa nimeweka katiba ya mwaka 2004 na 2006....Ukweli ni kwamba, Katiba ya 2006 Ilibadilishwa kinyemela by @UC Browser http://www.mpekuzihuru.com/2013/10/uozo-wa-chadema-wajulikanahapa-nimeweka.html?m=1
Jumanne, 29 Oktoba 2013
VIJANA WANACHUO KUTOKA VYUO VIKUU MJINI DODOMA KUWA MFANO KWA JAMII

Conrad na Justine ni vijana ambao kwa sasa wapo mwaka wa TATU na wa PILI katika vyuo vya DODOMA na St. JOHN, katika hali ya kushangaza vijana hao, wameanzisha mfomo wa kuwakopesha na kuwadhamini wanawake wajasiliamali wanaojikusanya katika makundi ya watu watano watano. wanawake hao, wanao patikana katika mtaa wa CHAMWINO katika Wilaya ya DoDOMA mjini, kweli hao ni vijana wa kuigwa katika hali ya kustajibisha kwa vijana walio wengi wa vyuoni hapa kwetu Tanzania wanao pewa Fedha za kujikimu na serikali wakati wa masomo yao ya juu na kuzitumia kwa kujirusha na kufanya Anasa zingine namwisho